Home Uncategorized JOSE MOURINHO ALIA NA VIUNGO WAKE KUMPONZA

JOSE MOURINHO ALIA NA VIUNGO WAKE KUMPONZA


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham amesema kuwa tatizo kubwa kwenye timu yake kwa sasa ni kukosa viungo sahihi wa kuichezesha timu yake ndani ya Uwanja.

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu England aliocheza Machi 7 dhidi ya Burnley alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Jambo lililomkasirisha Kocha huyo.

Burnley walianza kufunga dakika ya 13 kupitia kwa Chris Wood lilisawazishwa na Deke Alli kwa penalti dk ya 50.

Mourinho amesema kuwa kiungo wake Tanguay Ndombele alimtibulia mipango yake baada ya kumfanyia mabadiliko kipindi cha pili kwani mpango wake ilikuwa acheze dakika zote 90.

Mourinho ana kibarua kingine mbele ya RB Leipzig kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa jambo ambalo linampa wasiwasi wa kupenya kwenye mechi hiyo inayofuata.

Sare hiyo inaifanya Spurs kuwa nafasi ya sita kwenye Msimamo ikiwa na pointi 41 huku Burney wakiwa nafasi 10 na pointi 39 zote zimecheza mechi 29.

SOMA NA HII  KAZE ATANGAZA HALI YA HATARI YANGA