Home Uncategorized SABABU ZA MAULA KUKAA LANGONI LEO HIZI HAPA

SABABU ZA MAULA KUKAA LANGONI LEO HIZI HAPA

Simba ikiwa imecheza mechi 26, Manula amekaa langoni kwenye mechi 19 huku mechi saba akikaa mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya. Simba ikiwa imefungwa mabao 14 kati ya hayo tisa Manula ndiyo karuhusu.

Ametoka na clean sheet 12 ambapo ilikuwa ni mbele ya Kagera Sugar 0-3 Simba, Biashara United 0-2 Simba, Simba 1-0 Azam FC, Singida United 0-1 Simba, Simba 4-0 Mbeya City, Simba 0-0 Prisons, Ruvu Shooting 0-3 Simba, KMC 0-2 Simba, Mtibwa Sugar 0-3 Simba, Lipuli 0-1 Simba na Simba 1-0 Kagera Sugar, Simba 2-0 KMC.

Ametunguliwa kwenye mechi saba; Simba 3-1 JKT Tanzania, Simba 2-1 Mtibwa Sugar, Mwadui 1-0 Simba, Simba 0-1 JKT Tanzania, Simba 2-2 Yanga, Biashara United 1-3 Simba, Azam FC 2-3 Simba.

Dakika ZAKE.. Manula katika mechi 19 alizocheza na kufungwa mabao tisa amekuwa na uimara kila awapo langoni kutokana na uzoefu wake.

Amecheza dakika 1,710 akiwa kwenye lango na ana wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 190 alizokaa langoni.

Aina ya mabao aliyofungwa:


Ni mabao mawili amefungwa Manula na mshambuliaji aliye nje ya 18, alitunguliwa na Edward Songo wa JKT Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 3-1 na bao la pili lilikuwa mbele ya Mapinduzi Balama wakati Simba ikilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Yanga Uwanja wa Taifa Januari 4, 2020.

Kuzinguana na mabeki:


Manula amekuwa makini akiwa langoni na akifungwa anajitahidi kuwa na maneno ya kuwapa nguvu wachezaji wake, msimu wa 2018/19 wakati Simba ikifungwa na Kagera Sugar bao 1-0 ambalo lilikuwa la kujifunga kwa beki wake Mohamed Hussein rangi yake ya ukali ilionekana ila Erasto Nyoni aliweka usawa.

SOMA NA HII  SIMBA YAIBUKA NA JINGINE KUBWA LA USAJILI WIKI HII