Home Habari za michezo WAKATI WOWOTE SASA SIMBA WANAMTAMBULISHA KIPA HUYU

WAKATI WOWOTE SASA SIMBA WANAMTAMBULISHA KIPA HUYU

Tetesi za Usajili Simba

Klabu ya Simba wanatarajia muda wowote kumtangaza kipa raia wa Morocco, Ayoub Lakred, aliyehudumu takribani misimu minne katika klabu ya mabingwa wa Morocco msimu uliomalizika FAR Rabat.

Msimu uliopita ndiye aliyekuwa kipa namba moja wa FAR Rabat, akikaa langoni mara 31 ambapo mechi 25 kwenye ligi na 6 kombe la shirikisho wakiishia robo faibali.

Tangu ajiunge na FAR Rabat kutoka Berkane, amekuwa kipa kinara wa timu, amecheza mechi nyingi zaidi, katika nafasi hii amecheza mechi 100.

kocha wa zamani wa Simba Sven Vandebroeck, anahusishwa na ushawishi wa nyota huyu kujiunga na Simba.Kocha huyo alimfundisha kipa huyo wakati akiwa anaionoa timu FAR RABAT.

SOMA NA HII  MAXI NZEGELI ANABALAA WEWE, KIUNGO HUYU AFUNGUKA YALIYOWAKUTA JKT