Home Uncategorized MUUAJI WA SIMBA AMTAJA MKE WAKE KUHUSIKA KWENYE MABAO YAKE YOTE NDANI...

MUUAJI WA SIMBA AMTAJA MKE WAKE KUHUSIKA KWENYE MABAO YAKE YOTE NDANI YA YANGA


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anatupia mabao kutokana na maombi anayofanyiwa na mke wake pamoja na mwanae.

Morrisson ametua Yanga kwenye dirisha dogo la usajili ambapo ndani ya Ligi Kuu Bara amehusika kwenye mabao sita kati ya 31 yaliyofungwa na Yanga.

Amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao ambapo alikuwa mgeni wa kwanza msimu huu kwa wachezaji waliosajiliwa na Yanga kuitungua Simba, Uwanja wa Taifa Kwa bao 1-0.

Nyota huyo aliingia kwenye rada za Simba jambo lililowashtua Yanga na kumuongezea kandarasi ya miaka miwili kwa sasa ndani ya Wana Jangwani hao.


 “Mke wangu na binti wangu wamekuwa wakiniombea jambo ambalo linanipa nguvu ya kufunga kitu ambacho ninakipenda na kufurahia pia.

 “Binti yangu amekuwa akifurahi nikifunga sawa na mke wangu pia ananipa sapoti katika kazi yangu, sapoti ya mashabiki pia inachangia,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa ina mabao 31 ambapo kibindoni ina pointi 51.

SOMA NA HII  HIMID MAO:NILIPATA MUDA WA KUNUNUA MSOSI