Home news WAKATI WAKIJIANDAA NA SIMBA…NABI AIBUA MAPYA YANGA…BALAMA MAPINDUZI , ADEYUN WAHUSIKA…

WAKATI WAKIJIANDAA NA SIMBA…NABI AIBUA MAPYA YANGA…BALAMA MAPINDUZI , ADEYUN WAHUSIKA…


YANGA imeshinda mechi ya kirafiki kwa bao 1-0 dhidi ya Friends Rangers, lakini hiyo ishu. Mchongo mzima ulikuwa ni vile kocha Nasreddine Nabi, alivyokuwa akiisuka staili mpya ya kutaka kuwalaza mapema mahasimu wao Simba watakapokutana Desemba 11.

Straika Yusuph Athumani ndiye aliyefunga bao hilo pekee katika mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa kwenye uwanja wao wa mazoezi wa Avic Town, lakini kulikuwa na mambo mazito yanaendelea kiufundi kwa ajili ya mechi ya dabi ya Kariakoo.

Si unajua kwamba zimesalia siku nne kabla ya pambano hilo la watani wa jadi kupigwa pale Kwa Mkapa Jumamosi hii? Sasa unaambiwa kocha Nabi alikuwa bize kwelikweli kutengeneza staili mpya za mauaji.

Kocha Nabi katika kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri mchezo huo kwenye siku 7 za maandalizi alizokuwa nazo, aliomba kucheza mechi za kirafiki.

Nabi alitaka mechi za kirafiki ili kuwaweka wachezaji wake katika hali ya ushindani zaidi tofauti na wangekuwa wanafanya mazoezi bila ya kucheza mchezo wowote.

Mchezo wa kwanza wa kirafiki ndo huo wa juzi ambapo Nabi alijaribu mifumo mbalimbali kutoka ule wake wa 4-2-3-1 na kwenda mingine kama 3-5-2, 4-4-2 na mingine kutokana na mchezo ulivyokuwa ukiendelea.

Nabi alifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambao hupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza mara kwa mara na kuwapa nafasi wengine, lengo kubwa ni kupata 11, bora na wale watakaokuwa benchi kwenye mechi na watani zao Simba.

Beki wa kushoto wa Yanga, Adeyum Saleh alisema wao wachezaji wanatambua kila mchezo kwao ni fainali kwa kuwa wanahitaji pointi tatu kila mchezo ili wajiweke kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi na mbio za ubingwa msimu huu.

“Tutapambana kama tulivyopambana kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi na tukapata matokeo mazuri ya ushindi wa bao 1-0, tunawaheshimu Simba ni timu nzuri ila tutatumia vyema dakika 90,” alisema Adeyun na kuongeza;

“Mara zote mechi dhidi ya Simba haijawahi kuwa rahisi ndio maana tunafanya maandalizi ya kutosha aina mbalimbali ili kuwa bora dhidi yao na kufikia malengo yetu ya kupata ushindi.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUPOTEZA KATIKA MCHEZO ULIOPITA GAMONDI HATAKI UTANI TENA

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema wachezaji wote wapo kambini wakiwamo Mapinduzi Balama na Yassin Mustapha ambao tayari wote wapo fiti na wanafanya mazoezi kama wachezaji wengine.

Saleh alisema jukumu la kumtumia Balama au Mustapha lipo kwa kocha mkuu, Nabi kwani maendeleo yao ni mazuri zaidi na utimamu wa miili yao umeongezeka tofauti na siku za mwanzo waliporejea.

“Nabi ametuambia ndani ya siku hizi chache kabla ya kucheza na Simba anataka mchezo mwingine wa kirafiki ingawa bado hajafanya uamuzi timu ambayo angependa tucheze nayo,” alisema Saleh na kuongeza;

“Tunafanya yote hayo ili kuhakikisha tunakuwa na maandalizi na mbinu za kutosha kabla ya kukutana na Simba, kuhusu majeruhi ndani ya kikosi ni mmoja tu Yacouba Sogne ambaye si sehemu ya kikosi.”

Katika mchezo wa kwannza kukutana msimu huu, Yanga ilishinda 1-0, bao la straika Fiston Mayele katika mechi ya Ngao ya Jamii.