Home Uncategorized DROO YA KWANZA JISHINDIE GARI NI JUMATANO, ZAWADI KIBAO KUTOLEWA

DROO YA KWANZA JISHINDIE GARI NI JUMATANO, ZAWADI KIBAO KUTOLEWA

HATIMAYE ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa shauku kubwa na wanunuzi wa magazeti bora ya michezo Tanzania, Championi ambalo lipo mtaani kwa mia nane na SpotiXtra ambalo ni mia tano itafanyika Machi 25 na washindi kibao watasepa na zawadi zao.
Shindano hili ambalo ni shindano kubwa ambapo mshindi atajishindia gari limepokelewa kwa kishindo na wanunuzi wa magazeti ya michezo ambao mbali ya kufurahia habari na makala bora wanajiongezea nafasi ya kushinda zawadi kibao.
Akizungumza kuhusu mpango uliopo kwa sasa Meneja Mtendaji wa Global Group, Abdallah Mrisho, alisema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na lengo kubwa ni kurejesha shukrani kwa wasomaji wa magazeti yanayofanya vizuri sokoni.
“Tumeamua na tumedhamiria kuwa karibu na wasomaji kwa kuanza kwenye shindano letu kubwa la Jishindie Gari, droo ya kwanza inatarajiwa kufanyika Machi 25 ambayo itakuwa siku ya Jumatano.
“Ni rahisi sana kumpta mshindi na kushirki ni kununa gazeti lako la Championi au SpotiXtra kwa kadri uwezavyo hakuna kikokomo kwai unavyoshiriki zaidi unajiongezea nafasi ya kushinda gari.
“Droo ya Kwanza itakuwa ni kwa ajili ya kutafuta washindi wa Smart Phone, T Shirt na zawadi nyingine ndogondogo za papo kwa hapo, na kwa washiriki wanajiongezea nafasi ya kushinda zawadi kubwa ya gari jipya kabisa,” alisema.
Namna ya kushiriki
Nunua Gazeti la Championi au SpotiXtra, kasha fungua ukurasa wa pili ambao una maelekezo ya namna ya kushiriki bahati na sibu hiyo kwa kufuata maelekezo.
Namna ya kutuma
Kuponi iliyojazwa ambayo sio kivuli kwa maelekezo sahihi mpe muuza magazeti aliye karibu nawe popote pale ulipo au fika ofisi za Global Group, Sinza, Mori Dar kwa wale ama unaweza kutuma kwa njia ya sanduku la Posta, Jishindie Gari, Global Publisher, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
Kwa watoto chini ya miaka 18 hairuhusiwi kuchezwa na kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo zote.

SOMA NA HII  KISA CORONA, BEKI SIMBA AJIFUNGIA NDANI AKICHEZA GEMU