Home Uncategorized YUSUPH MHILU:NINAMSHUKURU MUNGU NINAENDELEA VIZURI

YUSUPH MHILU:NINAMSHUKURU MUNGU NINAENDELEA VIZURI

MTUPIAJI namba moja kwa wazawa ndani ya Ligi Kuu Bara,  Yusuph Mhilu amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa anaendelea vizuri kwa sasa.

Mhilu mwenye mabao 13 kibindoni na pasi tatu za mabao, jana, Julai 4 alishindwa kumaliza dakika 90 mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.

Dakika 90 zilikamika kwa timu hiyo kutoshana nguvu na Ruvu Shooting kwa kufungana bao 1-1. Mhilu alipata maumivu ya misuli ya nyama za paja.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri jambo analomshukuru Mungu.

“Nipo vizuri kwa sasa baada ya kupata huduma tofauti na ilivyokuwa awali hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu,” amesema.

Kugawana pointi mojamoja na Ruvu Shooting kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu Bara kumeifanya Kagera Sugar kufikisha jumla ya pointi 46 huku Ruvu ikiwa na pointi 43.

Zote zimecheza jumla ya mechi 33 ambapo Kagera Sugar ipo nafasi ya nane huku Ruvu ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. 

SOMA NA HII  MORRISON APEWA JEZI YA SANTOS