Home Uncategorized KOCHA SIMBA APEWA ONYO KALI NA BODI YA LIGI, POLISI TANZANIA WAVURUMISHWA...

KOCHA SIMBA APEWA ONYO KALI NA BODI YA LIGI, POLISI TANZANIA WAVURUMISHWA FAINI





Baada ya vituko kufululizo, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), imeonekana imepania kuweka sawa na kuhakikisha nidhamu inaboresha katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.


Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 10, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Ligi Kuu ya Vodacom:


Mechi namba 178: Simba SC 2 v Coastal Union  
FC  0

Kocha wa Simba Steven Vanden Broeck amepewa Onyo Kali kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na Kamishina wa mchezo wakati wa ukaguzi wa timu katika mechi hiyo iliyochezwa Februari  01,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.

Mechi namba 188: Simba SC 2 VS Polisi Tanzania FC 1

Klabu ya Polisi Tanzania imepigwa Faini ya kiasi cha Tsh.1,500,000/=(Milioni Moja na Laki Tano) kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa  Februari 04,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo
Vile vile katika mchezo huo Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Sc Steven VandenBroeck ametozwa Faini ya kiasi cha Tsh.500,000/=(Laki Tano) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 41(12) kuhusu Udhibiti wa Makocha.



SOMA NA HII  YANGA YATAJA MITAMBO YA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO