Home Uncategorized AZAM FC KUANZA KULISHUGHULIKIA TATIZO HILI MAPEMA NDANI YA TIMU YAO

AZAM FC KUANZA KULISHUGHULIKIA TATIZO HILI MAPEMA NDANI YA TIMU YAO


IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanyia marekebisho safu ya ushambuliaji ambayo imekuwa na shida kwenye umaliziaji.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wamekuwa wakitengeneza nafasi nyingi kwenye mechi zao ambazo wanazicheza ila wamekuwa wakishindwa kuzitumia.

“Tumekuwa tukitengeneza nafasi nyingi kwenye mechi zetu ila tatizo lipo kwenye umaliziaji hilo ndilo tunalifanyia kazi kwa sasa,” amesema.

Obrey Chirwa ndiye kiongozi wa safu ya ushambuliaji ya Azam FC ametupia mabao nane kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURAAA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO