Home Habari za michezo KIEMBA AFAFNUKIA KISA CHA AL AHLY KUJA NA MAPIPA

KIEMBA AFAFNUKIA KISA CHA AL AHLY KUJA NA MAPIPA

kiemba

Wakati Mashabiki wa soka nchini wakishangazwa na ujio wa Al Ahly ambao wanjiandaa kuikabili Simba siku ya Ijumaa Oktoba 20.

Mchambuzi wa Soka kutoka Clouds FM anasema jambo hilo sio la kushangaza kwa vilabu ambavyo vimeendelea.

Akizungumza Kiemba anasema;

“Al Ahly kuja na mapipa sio kama hawajiamini ,ni sehemu ya maandalizi hawahitaji sababu iwe ni kukosekana kwa kitu fulani ,mchezo wa mpira wa miguu kichwa ndio nguzo ,mwili ni kama chepe kwenye kuchotea likiwa lenyewe haliwezi na wao hawataki usumbufu ndio maaan wamekuja na kila kitu kipo kwenye mstari “

“Na hii ni kuonyesha kwamba wenzetu wapo mbali sana, wenzetu tangu miaka ya nyuma wanalifanyia kazi kwamba eneo la ubongo ni eneo muhimu sana kwenye mapambano ya mpira wa miguu , mimi naona sio uoga isipokuwa ni utaratibu ndio unavyotaka kwa timu “

SOMA NA HII  NABI AIPUUZA SIMBA....AKACHA MAANDALIZI YA DABI...ARINGIA UBORA WA KIKOSI...