Home Habari za michezo HAPO SIMBA NI FULL MZIKI, BOCCO AFUNGUKA

HAPO SIMBA NI FULL MZIKI, BOCCO AFUNGUKA

Habari za Simba SC

Nahodha wa Simba ya Dar es Salaam, John Bocco amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri kukabiliana na Al Ahly ya Misri mchezo wa ufunguzi michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) kesho Oktoba 20, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Pia, amesema kurejea kikosini kwa beki Henock Inonga kumezidi kuimarisha timu yao kwa ajili ya mchezo huo.

“Utakuwa ni mchezo mkubwa kwa Afrika yetu na Tanzania kwa ujumla, tunategemea kuonesha mchezo mzuri na wa kiungwana kwa wapinzani wetu,” amesema Bocco.

“Mchezo utakuwa mgumu lakini mwalimu ametuandaa vizuri na tunaomba mashabiki washirikiane nasi. Tunatarajia matokeo mazuri kwani tuna wachezaji wazuri wenye ubora na uzoefu kucheza michezo ya aina hii katika kikosi chetu,” amesema nahodha huyo.

“Tuna wachezaji wazuri na tumefurahi kurejea kikosini kwa mwenzetu, Henock Inonga baada ya kuwa majeruhi kwa majumaa kadhaa, na bila shaka yupo tayari kwa mchezo wa kesho, kinachobaki ni mipango tu ya mwalimu na benchi lake la ufundi,” amesema Bocco.

SOMA NA HII  SIMBA NA CHAMA SASA ISHU IKAE HIVI TU