Home Habari za michezo HIVI HAPA VYUMA VIPYA VITATU VINAVYOTUA YANGA DIRISHA DOGO….SIMBA WAKIJISAHAU IMEKULA KWAO…

HIVI HAPA VYUMA VIPYA VITATU VINAVYOTUA YANGA DIRISHA DOGO….SIMBA WAKIJISAHAU IMEKULA KWAO…

Habari za Yanga leo

Ikiwa imetinga hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inajipanga kusajili wachezaji wapya watatu katika usajili wa dirisha dogo kwa lengo ya kuhakikisha wanafanya vyema zaidi katika michuano hiyo ya kimataifa, imefahamika.

Yanga imedhamiria kuimarisha kikosi chake kwa sababu wanaamini itawasaidia kufanya vizuri katika vita ya kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na taji la Kombe la FA ambayo wanayashikilia.

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa rasmi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ifikapo Desemba.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema huenda uamuzi wa kusajili wachezaji hao wapya umetolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye anataka kuona kila idara inakuwa imara na hatimaye wanafikia malengo.

Chanzo hicho kiliendelea kusema Gamondi anahitaji kupata straika mpya mmoja na nafasi nyingine mbili zitakazobainika zinahitaji kuongezewa nguvu.

Taarifa zaidi ziliendelea Gamondi amehitaji kuongeza nguvu baada ya kubaini ndani ya kikosi chake kuna aina tatu ya wachezaji.

“Kocha amesema kwa sasa kuna wachezaji wanaojituma kweli kweli na kuifanya Yanga, pili kuna wachezaji wazuri lakini wanategea mazoezi na tatu ni wale ambao amedai hawastahili kuwamo na kuichezea timu kubwa kama Yanga,” kilisema chanzo chetu.

Kiongozi huyo alisema kwa sababu hiyo, Gamondi anadaiwa kutaka kuondoa wachezaji ambao hawana faida na timu na anaamini wapya watakaosajiliwa watashirikiana na wenzao waliopo ili kuipambania timu hiyo.

“Unajua kikosi kwa sasa kimebaki na baadhi ya wachezaji tu, wengine wamekwenda kuzitumikia nchi zao kwenye timu za taifa kwa hiyo waliobaki amekuwa wakiwaangalia kwa ukaribu zaidi, nafasi hii inamsaidia kuwajua wachezaji ambao mpaka sasa bado hawajaonyesha kitu chochote au kumshawishi,” chanzo chetu kiliongeza.

Hata hivyo, chanzo chetu kilisema kabla ya Gamondi kukamilisha zoezi la kutaja majina ya wachezaji asiowahitaji, ametoa mechi nne kwa baadhi ya wachezaji ili kukamilisha mchakato wake.

“Kocha anasema anataka wachezaji walio tayari kuipambania Yanga na kuifikishia malengo yake, ameshakaa na wachezaji ambao wanaona hawatimizi wajibu wao na kuzungumza nao, kipindi cha dirisha dogo huenda akapendekeza tukasajili straika mmoja na wachezaji wengine wawili kwenye nafasi nyingine tofauti,” aliongeza mtoa habari wetu.

Wakati huo huo, uongozi wa Simba umesema kikosi chao kinaendelea vyema na mazoezi na wanaamini malengo yao ya kuweka historia msimu huu katika michuano ya kimataifa wanayoshiriki yatatimia.

“Hata Al Ahly wanaifahamu Simba na hawataona kitu kipya tukiwafunga hapa nyumbani kwa sababu tuliwahi kufanya hivyo, safari hii tumejipanga kutaka kuwatoa kwenye mashindano hayo kwa kuwafunga hapa na kwao kwenye mchezo wa marudiano,” alisema Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba.

Aliongeza benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ limeendelea kukisuka kikosi chao na ametamba tayari ameanza kutengeneza ‘dawa’ ya kuwaondoa Al Ahly katika mashindano hayo.

“Kikosi kipo kambini kwa wachezaji ambao hawako katika majukumu ya timu za taifa, wale majeruhi tayari wanaendelea vizuri akiwamo beki yetu, Henock Inonga ambaye ameitwa katika kikosi cha DRC, Manula (Aishi) amerejea vizuri kwenye mazoezi,” alisema meneja huyo.

Simba imeifunga Al Ahly mara zote inapokutana nayo hapa nchini, tatizo linakuwa inapokwenda ugenini nchini Misri.

Mwaka 1984, Simba iliifunga Al Ahly mabao 2-1, mechi ikichezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ikiwa ni Kombe la Washindi Barani Afrika (sasa Kombe la Shirikisho), kwa mabao ya Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ na Mtemi Ramadhani, lakini ikapoteza kwa magoli 2-0 ilipokwenda Cairo na kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2.

Zilikutana tena mwaka 2019 katika wa kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikipigika nchini Misri mabao 5-0, lakini ikashinda nyumbani bao 1-0, shukrani Meddie Kagere na mwaka 2021 Simba iliichapa tena Al Ahly hapa nyumbani bao 1-0 kupitia Luis Miquissone katika mechi ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini ikafungwa tena ugenini goli 1-0.

SOMA NA HII  SASA AZIZ KI NA ISHU YA KIATU CHA UFUNGAJI BORA LIGI KUU