Home Uncategorized HIVI NDIVYO CAF WALIVYOTIBUA MIPANGO YA SIMBA

HIVI NDIVYO CAF WALIVYOTIBUA MIPANGO YA SIMBA

CRESCENTIUS Magori, Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba amesema kuwa ratiba ya michuano ya kimataifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) imesababisha wapangue ratiba zao zote.

Magori amesema kuwa mwaka huu wamebadili ratiba  ya maadhimisho ya Simba day kutokana na ratiba kubana,kwani mechi yao ya kwanza kimataifa dhidi ya UD Songo itakuwa Agost 10.

“Tumeamua kubadili ratiba zetu zote baada ya Caf kutoa ratiba za awali, tumerudisha tarehe ya mechi nyuma mpaka sita tulipanga iwe tarehe 3 ambayo ni wikend ila  kuna wachezaji wetu wapo timu ya Taifa hivyo hatuwezi kufanya jambo lolote.

“Ratiba ya michuano kubadilika imetufanya tubadili ratiba kwani tulipanga kucheza Dar, Mwanza ila sasa mambo yamekuwa magumu hatuna nafasi, labda mwakani tunaweza kufanya hivyo.

“Tamasha hili lipo kwenye mipango na vyanzo vya Simba hivyo wakati mwingine itakuwa ni kubwa kuliko sasa na bajeti yake itakuwa kubwa na mipango inazidi kuiva na tunaifanyia kazi,” amesema.

Agosti 6 Simba itacheza na Power Dyanamo kwenye kilele cha Simba day ambayo huwa maalumu kwa ajili ya kutambulisha jezi mpya pamoja na wachezaji wa Simba.

SOMA NA HII  HASIRA ZA LUKAKU BADO ZINAWAKA KWA KOCHA WAKE