Home Yanga SC TAMBWE:BADO SIJALIPWA BADO NA YANGA

TAMBWE:BADO SIJALIPWA BADO NA YANGA


 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amefunguka kuwa Yanga bado hawajamlipa fedha zake anazodai Sh milioni 42 licha ya siku 45 walizopewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kumalizika.


 Tambwe ametoa kauli hiyo baada ya siku 45 zilizotolewa na Fifa kumalizika bila kuwepo kwa dalili za malipo hayo.

 

Tambwe amesema mpaka sasa hajua chochote juu ya malipo ya fedha zake kutoka Yanga licha ya kuwapa hesabu zote kwani hata wakili wake, Felix Majani hajui lolote kutoka ndani ya timu hiyo licha ya siku walizopewa kumalizika.

 

“Binafsi hakuna ambacho kwa sasa najua kutoka Yanga zaidi ya kwamba bado hawajanilipa licha ya kupigiwa simu na Injinia, Hersi Saidi na kuniambia nifanye mahesabu ya pesa ambazo nawadai, mwanasheria wangu amefanya hivyo, akawatumia lakini hakuna jambo lolote jipya.

 

“Ninachojua kwamba Fifa waliwapa siku 45 wawe wameshalipa lakini hadi sasa zimeisha na hakuna lolote, hivyo hawezi kufanya usajili wowote katika usajili ujao hadi wawe wamelipa na kuwasiliana na mwanasheria wangu ili arudishe taarifa Fifa,” amesema Tambwe.


Chanzo:Championi


SOMA NA HII  AUCHO AWAGEUKIA WACHEZAJI..."MKITAKA NIWE MTU MBAYA NITAFANYA HIVYO