Home Uncategorized STARS WAPEWA CHAPUO KUTUSUA AFCON

STARS WAPEWA CHAPUO KUTUSUA AFCON


SAMUEL Etoo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Cameroon,Barcelona, Chelsea na Inter Milan amesema kuwa Stars ina nafasi ya kufanya maajabu endapo wachezaji watajituma.

“Nimeshangazwa kuskia kwamba Tanzania inashiriki michuano ya Afcon baada ya kupita miaka mingi kushiriki wakati nacheza na timu ya Tanzania nilikuwa napambana na wachezaji wenye vipaji.

“Ila kwa kuwa kwa sasa wamepata nafasi ya kushiriki naamini watafanya maajabu kwenye michuano ya Afcon kutokana na aina ya timu waliyonayo pamoja na vipaji ambavyo vipo Tanzania endapo wachezaji watajituma,” amesema Etoo.

Stars kwa sasa ipo nchini Misri ilipoweka kambi ambapo kazi kubwa ya maandalizi imeanza na jana walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri na walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


SOMA NA HII  SIMBA, YANGA MMBO YAMESHAANZA TENA HUKO WPL