Home Uncategorized ISHU YA UBUTU WA USHAMBULIAJI YANGA INAFANYIWA KAZI

ISHU YA UBUTU WA USHAMBULIAJI YANGA INAFANYIWA KAZI


 JUMA Mwambusi, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa tatizo la washambuliaji ndani ya kikosi chake kwa sasa wanalifanyia kazi ili kuongeza uimara katika kikosi hicho.


Yanga ikiwa imecheza mechi 11 safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 13 huku safu ya ulinzi ikiwa imefungwa mabao manne.


Novemba 25 ina kibarua cha kumenyana na Azam FC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 25 ikiwa kwenye nafasi hiyo kwa tofauti ya mabao ya kufunga, ambapo vinara hao wa ligi wamefunga mabao 18 na kufungwa mabao matano.


Mwambusi amesema:”Suala la kutokufunga mabao hilo lipo na tunalifanyia kazi, imani yetu ni kwamba tutaanza kupata matokeo kwenye mechi zetu zijazo kwa kuwa wachezaji wanafuata maelekezo na kila mmoja anatambua majukumu yake,” .


Kinara wa utupiaji ni Michael Sarpong mwenye mabao matatu na anafuatiwa na Carlos Carlinhos ambaye ni kiungo mwenye mabao mawili sawa na Lamine Moro ambaye ni beki.

SOMA NA HII  SIMBA KWENYE LIGI KUU BARA WAMEKUMBUKA HIKI HAPA