Home Uncategorized LIVERPOOL YAWEKA REKODI YAKE ANFIELD

LIVERPOOL YAWEKA REKODI YAKE ANFIELD

 


USHINDI wa mabao 3-0 walioupata Liverpool usiku wa kuamkia leo dhidi ya Klabu ya Leicester City,  Uwanja wa Anfield unawafanya waweke rekodi ya kucheza jumla ya mechi 64 bila kufungwa kwenye Uwanja wao huo wa nyumbani. 


Kwenye jumla ya mechi 64, Liverpool imeshinda mechi 53 na kulazimisha sare 11 huku ikusanya jumla ya mabao 169 na imefungwa mabao 42 na ushindi wao mkubwa ilikuwa ni wa mabao 5-0 kwa timu nne ambazo ni Swansea, Watford mara mbili na Huddersfield. 


Mabao ya mchezo dhidi ya Leicester City iliyo kwenye ubora wake yalifungwa na Jonny Evans dakika ya 21 alijifunga, Diogo Jota alipachika la pili dakika ya 41 na lile la tatu lilipachikwa na Robert Firmino dakika ya 86.

Licha ya kuwa na lundo la wachezaji wake muhimu ambao wapo nje ya kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na Virgil van Dijk Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp imeweza kuingia ndani ya tatu bora baada ya kufikisha pointi 20 sawa na Tottenham Hotspur inayoongoza Ligi Kuu England.

SOMA NA HII  BREAKING: SENZO ANAFUNGUKA YOTE, KILICHOMTOA SIMBA, NAFASI YAKE YANGA - "SIJUTII MAAMUZI YANGU"