Home Habari za michezo GAMONDI ATAMBA KUICHAKAZA ASAS KESHO, HUKU AKIJITETEA HIVI

GAMONDI ATAMBA KUICHAKAZA ASAS KESHO, HUKU AKIJITETEA HIVI

Habari za Yanga SC

Kesho Agosti 20 katika Uwanja wa Azam Complex utachezwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika mchezo utakaowakutanisha mabingwa wa Ligi ya Djibouti ASAS na mabingwa wa Ligi ya Tanzania Yanga.

Miguel Gamondi kocha wa Yanga amesema wamejipanga vizuri kwa mchezo huo licha ya kutokujua uimara na udhaifu wa wapinzani wao.

Gamondi amesema yeye ni kocha mpya na anatamani kuweka historia yake mpya kwasababu Yanga haijaingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika miaka ya hivi karibuni.

“Tumejipanga vizuri, hatumfahamu mpinzani kiundani lakini tumejipanga kufanya vizuri na kuandika historia mpya”

SOMA NA HII  RAISI WA YANGA AFUNGUKA HAYA KUHUSU USAJILI WA MSIMU HUU