Home Habari za michezo USAJILI WA KWANZA WA MBRAZILI NDANI YA SIMBA WATIKI…KULIPWA ZAIDI YA MIL...

USAJILI WA KWANZA WA MBRAZILI NDANI YA SIMBA WATIKI…KULIPWA ZAIDI YA MIL 248 …

Habari za Simba SC

ISMAEL Sawadogo kiungo mkabaji raia wa Burkina Faso ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Simba.

Kuiungo huyo ambaye ni Ni raia wa Burkina Faso alizaliwa mwaka1996 anakuwa usajiliwa kwanza kabisa wa Kocha Robertinho ambaye inasemwa kuwa ndiye aliyempendekeza.

Sawadogo Alikuwa anakipiga Klabu ya Difaa Hassani El Jadid. amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili, huku ikitajwa kuwa mshahara wake kwa mwezi utakuwa dola 4500 sawa na Tsh zaidi ya Milioni 10,
Anakuja kuchukua mikoba ya Victor Ackpan ambaye atatolewa kwa mikopo.

Tetesi za Usajili SimbaAckpan raia wa Nigeria amekwama kufiti kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na kuanza msimu akisumbuliwa na majeraha na hata aliporejea kwenye ubora wake bado hakuwa imara.

Juma Mgunda, kocha msaidizi wa Simba aliweka wazi kuwa nyota huyo atakuja kuwa imara taratibu kwenye kikosi hicho.

Kwa sasa Ackapn hayupo na timu nchini Dubai ambapo imeweka kambi kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa anafuatilia masuala ya hati yake ya usafiri.

Anakuwa nyota wa pili kutambulishwa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuanza na Said Ntibanzokiza ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Geita Gold.

SOMA NA HII  KIGOGO YANGA NAYE ASHINDWA KUJIZUA..ATEMA NYONGO KISA TIMU KUBORONGA KIMATAIFA...