Home news WAKATI DILI LA CHAMA KUTUA SIMBA LIKIWA TAYARI…UONGOZI WAANIKA SIKU YA KUMTAMBULISHA…

WAKATI DILI LA CHAMA KUTUA SIMBA LIKIWA TAYARI…UONGOZI WAANIKA SIKU YA KUMTAMBULISHA…


UONGOZI wa Simba SC, umepanga kumtambulisha Clatous Chama siku ya mwisho kabla ya usajili wa dirisha dogo haujafungwa Januari 15, mwaka huu.

Chama ambaye aliitumikia Simba kwa misimu mitatu, aliondoka kikosini hapo mwishoni mwa msimu wa 2020/21 na kutimkia RS Berkane ya Morocco.

Kwa muda mrefu, kumekuwa na tetesi za Simba kuhitaji kumrudisha kundini kiungo huyo wa Zambia ambaye inasemekana hana furaha ndani ya RS Berkane.

Chanzo kutoka katika kambi ya Simba iliyopo Zanzibar, kimeliambia Spoti Xtra kwamba: “Chama ameshamalizana na viongozi na muda si mrefu tutampokea Dar, hii ni baada ya kumaliza majukumu yetu ya Kombe la Mapinduzi.

“Baada ya kumpokea Chama, viongozi wamepanga kumtambulisha siku ya mwisho kabisa ya usajili.” Kwa upande wa Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alizungumzia ishu hiyo akisema:

“Baada ya Kombe la Mapinduzi, tukutane Uwanja wa Julius Nyerere jijini Dar, tuna jambo letu. Siwezi kusema moja kwa moja ni Chama, ila mashabiki wa Simba watafurahi sana.”

SOMA NA HII  MORRISON AWAPANIA WABOTSWANA KESHO....ATOA AHADI HII MPYA ...