Home Ligi Kuu YANGA KULITETEA TAJI LAO…TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA…TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE

YANGA KULITETEA TAJI LAO…TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA…TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE

YANGAKULITETEA TAJI LAO...TUMEWAACHA POINTI NYINGI WANAOTUFATA...TUNAPAMBANIA MATAJI YOTE

Pointi 8 ambazo wamewaacha watani zao wa jadi Simba, zimeipa kiburi Yanga ya kufanya vizuri kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu Bara na kutetea taji lao.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 65, huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 57, zote zikiwa zimecheza mechi 24.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga, alisema: “Ni pointi nyingi ambazo tumewaacha wale wanaotufuata, bado tuna mechi mbele yetu, tutapambana kushinda zote ili kutetea taji letu.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya kupambania mataji ambayo tunatetea ikiwa ni pamoja na ligi, hili ni muhimu kwetu ukizingatia tunaongoza katika msimamo, tunaamini kwamba tutafikia malengo yetu.”

SOMA NA HII  HABARI ZA USAJILI...SIMBA YATUA KWA MSHAMBULIAJI WA STELLA ADJAME...YANGA NA OKRAH