Home Simba SC SIMBA QUEENS WAKABIDHIWA NDINGA MPYA

SIMBA QUEENS WAKABIDHIWA NDINGA MPYA

Klabu ya Simba Queens leo Jumatatu ilikabidhiwa basi jipya aina ya Costa kwa ajili ya safari za timu ndani na nje ya mkoa.

Hafla ya kukabidhiwa gari hiyo ilifanyika kwenye ofisi za Africarries zilizopo Vingunguti jijini Dar es salaam na basi hilo limetolewa na kampuni hiyo ikiwa kama sehemu ya udhamini kwa klabu hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo Mkuu wa Kitengo Cha Sheria cha Africarries Ngassa Mboje alisema basi hilo wamelitoa ikiwa kama sehemu ya kudumisha ushirikiano na klabu hiyo.

“Huu ni mwanzo mzuri wa ushirikiano baina yetu na Simba Queens pamoja na mlezi wa Simba Fatema Dewji ikiwa kama sehemu ya juhudi za kuwaunga mkono na kuwapa nguvu Wanawake,” alisema Ngassa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa basi kwa ajili ya Simba Queens, mlezi wa timu hiyio, Fatema Dewji aliwashukuru Africarriers Limited kwa kuidhamini timu yao na kuwapatia basi aina ya Coaster.

“Japo kuwa udhamini umekuja ukingoni mwa msimu , nina imani itakuwa chachu ya kutetea ubingwa wetu na utaendelea hadi msimu ujao kwani mchango kama huu ni chachu kwenye soka la wanawake nchini,” alisema Fatema.

Alisema Simba Queens inawaahidi Africarrier na mashabiki wote kutetea ubingwa wake na kurudi na kombe katika mchezo utakaochezwa Mei 13 jijini Dodoma dhidi ya Baobab Queens.

Naye Mkurugenzi wa Africarrier Ltd, Mohamed Raza Pirbhal alisema anaamini katika maendeleo ya wanawake na Simba Queens na kuahidi kuendelea kuisaidia klabu hiyo iliyopo kwenye mbio za kutetea ubingwa wa msimu huu.

“Tumetoa basi hili kwa ajili ya kuwasaidia usafiri wa kwenye kwenye michezo yenu lakini endapo mtwatwaa ubingwa kuna zawadi yenu maalumu,” alisema Raza.

SOMA NA HII  MOGELLA:- CHAMA ANAENDELEZA UFALME WAKE SIMBA SC...HATA OKWI ALIFANYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here