Home Ligi Kuu KMC:TUTAYEYUSHA PIRA ICE CREAM LA AZAM FC

KMC:TUTAYEYUSHA PIRA ICE CREAM LA AZAM FC


UONGOZI wa KMC umeweka wazi kwamba utawafuata wapinzani wao Azam FC kwa lengo moja tu la kwenda kuyeyusha pira Ice Cream ambalo wanatamba nalo kwa sasa.


KMC imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana na Namungo FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa jana, Mei 9, Uwanja wa Majaliwa.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa tayari timu imerejea na kesho itaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam FC.

“Tumerejea salama leo kutoka Ruangwa, mkoani Lindi ambapo tulikuwa na mchezo dhidi ya Namungo.

Kupata sare ya bila kufungana kwetu sio mbaya licha ya kwamba tulikuwa tunahitaji ushindi.

“Kesho wachezaji wataanza kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC.
Mtakumbuka kwamba Azam FC ipo nafasi ya tatu na sisi tupo nafasi ya tano, tunafanya maandalizi kwenda kuyeyusha Ice Cream.

“Mchezo wa kwanza tulipokutana nao Uwanja wa Uhuru tulipata pointi tatu hivyo tunawaambia wapinzani wetu kwamba tumerudi na tupo imara,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 15, Uwanja wa Azam Complex.
SOMA NA HII  MAISHA YANAKWENDA KASI, MAPAMBANO LAZIMA YAENDELEE