Home kimataifa REAL MADRID YAIPIGIA HESABU SAINI YA KANE WA SPURS

REAL MADRID YAIPIGIA HESABU SAINI YA KANE WA SPURS

 IMERIPOTIWA kuwa mabosi wa Real Madrid wamewaambia viongozi wa Tottenham kwamba chaguo lao la kwanza kwenye usajili ni mshambuliaji wao Harry Kane ili ajiunge na kikosi hicho msimu ujao.

Mabosi hao wa Hispania wapo kwenye hesabu za kumsaka mshambuliaji daraja la kwanza pale msimu wa 2020/21 utakapomeguka na wanaamini kwamba Kane ni chaguo sahihi kwao ikiwa watapata saini yake.

Mbali na Kane pia inaelezwa kuwa Real Madrid wanavutiwa na uwezo wa mshambuliaji wa kikosi cha Paris Saint-Germain, (PSG), Kylian Mbappe na ikiwa watamkosa basi wataongeza nguvu kumsaka nyota wa Borussia Dortmund, Erling Haalad.

Ripoti zimeeleza kuwa Real Madrid wanaamini kwamba makubaliano ya kumpata Kane ni rahisi kwao na yanawezekana tofauti na kupata saini ya Mbappe ama Haalad.

Madrid chini ya Zinedine Zidane inahitaji kuboresha kikosi hicho huku wakiamini kwamba kumpata Kane ambaye ni nyota ndani ya Tottenham inayonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho akiwa amecheza jumla ya mechi 377 na kufunga mabao 215 ndani ya misimu nane ni moja ya sifa imara kwake.


SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED WAPO TAYARI KUMSIKILIZA de GEA