Home Ligi Kuu MECHI YA SIMBA V COASTAL UNION YAOTA MBAWA, KUPANGIWA TAREHE

MECHI YA SIMBA V COASTAL UNION YAOTA MBAWA, KUPANGIWA TAREHE



 MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Coastal Union dhidi ya Simba umeahirishwa kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB).

Taarifa hiyo imeeleza namna hii:”Mchezo wa VPL na.259, (Simba vs Coastal Union) uliopangwa kuchezwa Mei 11,2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, umeahirishwa na utapangiwa tarehe nyingine kwa sababu Simba inalazimika kusafiri siku hiyo kwenda A.Kusini kwa ajili ya mchezo a CAFL dhidi ya Kaizer Chhiefs Mei 14,”. 

Rekodi zinaonyesha kwamba mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilisepa na pointi tatu mazima.

Baada ya dakika 90, ubao ulisoma Coastal Union 0-7 Simba na nahodha John Bocco alisepa na mpira baada ya kufunga hat trick.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YATAKA TANO BORA