Home Simba SC SIMBA YAVUNJA REKODI YAKE ILIYOWEKA KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

SIMBA YAVUNJA REKODI YAKE ILIYOWEKA KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 


KLABU ya Simba imevunja rekodi yake kwenye mashindano yanayoandaliwa na Kombe la Shirikisho Afrika, (Caf) kwa kuvunja rekodi kwenye hatua za makundi baada ya mechi nne.


Msimu wa 2018/19 ikiwa chini ya Patrick Aussems wengi wanapenda kumuita Uchebe baada ya kucheza mechi 4, ilishinda mbili na kupoteza mbili bila kuambulia sare. Msimu huu wa 2020/21 imeipindua kwa kushinda mechi tatu na kuambulia sare moja.

Kwa upande wa mabao ya kufunga msimu wa 2018/19 ilifunga mabao manne na msimu huu wa 2020/21 imefunga jumla ya mabao matano.

Pia ilikusanya mzigo wa mabao 10 baada ya mechi nne ila msimu huu baada ya mechi nne ukuta wao haujaokota bao nyavuni ambapo una clean sheet nne tofauti na msimu wa 2018/19 ilipokuwa na clean sheet mbili na ilikuwa nafasi ya 2 na pointi 6 ila msimu huu ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 10.

Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakipambana muda wote jambo linalowapa matokeo chanya.

“Wachezaji wanajua majukumu yao na muda wote nimekuwa nikiwaambia kwamba wanapaswa kutimiza kile ambacho tunakihitaji, bado tuna kazi ya kufanya mashabiki wazidi kutupa sapoti,” .

SOMA NA HII  SIMBA MAMBO YAANZA KUJIPA HUKOOO....BENCHIKHA HATAKI MZAHA UNAAMBIWA...