Home Habari za michezo SIMBA MAMBO YAANZA KUJIPA HUKOOO….BENCHIKHA HATAKI MZAHA UNAAMBIWA…

SIMBA MAMBO YAANZA KUJIPA HUKOOO….BENCHIKHA HATAKI MZAHA UNAAMBIWA…

Habari za Simba leo

WACHEZAJI wa Simba wakiwemo nyota wapya waliosajiliwa kipindi cha dirisha dogo la usajili na wale walikuwepo wanayarajia kuingia kambiniĀ  kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kikosi cha Simba kinachonolewa Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha kinaingia kambini kikiwa na kazi moja tu ya kurudisha heshima yake kama klabu ya kuogopwa na timu mbalimbali za Afrika.

Meneja Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kikosi kimerejea kwenye mazoezi na kujiandaa michezo iliyopo mbele yao kufanya vizuri katika mechi za ligi na kimataifa.

Amesema wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa na wale waliosajiliwa kipindi cha dirisha dogo kuanza kazi rasmi katika majukumu yao mapya.

“Baada ya mapumziko mafupi, kikosi kimeanza rasmi mazoezi , Mtaalamu wetu Benchikha amekuja kwa ari kubwa na kuhakikisha anaandaa kikosi kuwa imara na tishio.

Wachezaji wapya ni hatari na kazi kubwa ambayo kocha anaifanya ni kutengeneza muunganiko mzuri hasa safu ya ushambuliaji, ukizingatia tumeleta kina Freddy Michael, Pa Omar Jobe na wengine,” amesema Ahmed.

Amesema mazunguko wa pili wanakuja kivingine kwa sababu mipango ya benchi la ufundi ni kuona timu inapata matokeo mazuri katika ligi, FA na michuano ya kimataifa.

Baada ya mapumziko hayo, Simba itacheza Februari 17, mwaka huu dhidi ya Dodoma Jiji mchezo wa Ligi Kuu Bara, katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 ilizovuna katika michezo kumi iliyocheza, imeshinda michezo saba, imetoka sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.

SOMA NA HII  MABOSI LIGI KUU WAMPIGIA SALUTI BALEKE...ASHINDA TUZO HII KUBWA BONGO