Home Habari za michezo BAADA YA KUONEWA ‘ROUND’ YA KWANZA …SIMBA NA YANGA ZAANZA KUJIPATA MDOGO...

BAADA YA KUONEWA ‘ROUND’ YA KWANZA …SIMBA NA YANGA ZAANZA KUJIPATA MDOGO MDOGO..

Habari za michezo

MECHI tisa za Ligi ya Vijana chini ya miaka 20 zimezibeba Yanga na Simba kutoka mkiani na kusogea nafasi tano za juu baada ya kuanza kwa kusuasua.

Timu hizo zilianza kwa kupoteza michezo ya mwanzo na kukaa mkiani mwa ligi hiyo, lakini michezo ya hivi karibuni imezirudisha kwenye njia na sasa Yanga ipo nafasi ya tatu na Simba ya tano.

Kila timu inacheza mechi 14 – saba za raundi ya kwanza na nyingine ile ya pili, kisha zinatafuta nane bora ambapo kila kundi linatoa timu nne.

Mpaka sasa Azam FC ndiyo vinara wa Kundi A, ikicheza mechi tisa na kukusanya pointi 20, huku Coastal Union ikiwa na pointi 17, Yanga 12, Ihefu 12, Simba tisa, Tanzania Prison nane sawa na Namungo ilhali KMC ikishika mkiani na pointi saba.

Dodoma Jiji inaendelea kusalia kileleni mwa Kundi B ikikusanya pointi 24, Mtibwa Sugar pointi 21, JKT Tanzania alama 14, Mashujaa 12, Singida FG na Kagera Sugar zikilingana pointi nane, Geita Gold pointi saba na Tabora United ikiwa nazo tano.

Msimamo huo unakuja baada ya mechi za juzi Kundi A ambapo Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Namungo 2-0 KMC, Azam FC 2-0 Ihefu.

JKT Tanzania iliifumua Kagera Sugar 3-1, Mtibwa Sugar ikailamba Tabora United 2-1, Dodoma Jiji ikiiosha Mashujaa 3-2.

Kocha Mkuu wa Yanga, Vicent Barnabas alisema matokeo waliyopata juzi dhidi ya watani wao si mabaya, lakini watawekeza nguvu zaidi ili kushinda mechi ijayo dhidi ya Coastal.

“Tunacheza mwezi ujao jijini Tanga. Sio mechi rahisi kupambana na timu iiliyopo nafasi ya pili, lakini naamini tutapata muda mwingi wa kujiandaa ili tujiweke pazuri,” alisema Barnabas.

Kocha wa Simba, Mohamed Mulishona ‘Xavi’ alisema kuna mabadiliko ya kikosi katika raundi ya pili na mipango yao ni kushinda kila mechi ili kwenda hatua inayofuata.

“Raundi ya kwanza tulicheza vibaya lakini sasa hivi timu ina muunganiko naiona ikisogea hadi nafasi ya juu. Kikubwa tunapambana kushinda kila mechi na ijayo tutacheza na Prisons, nafikiri tutafanya vizuri ,” alisema Xavi. Ligi hiyo itaendelea Februari 7 pale Yanga itaumana na Coastal Union huku Simba ikikutana na Prisons.

SOMA NA HII  BAADA YA KUJIUNGA NA YANGA...MUDATHIRI ATAJA NAFASI ZA AUCHO NA SURE BOY...

1 COMMENT