Home epl CHELSEA WALIPA KISASI MBELE YA LEICESTER CITY

CHELSEA WALIPA KISASI MBELE YA LEICESTER CITY

 

KLABU ya Chelsea inayofundishwa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel imelipa kisasi mbele ya Leicester City ambao walitwaa Kombe la FA kwenye fainali ambayo walikutana nao Mei 15.

Katika fainali hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa ubao wa Stamford Bridge ulisoma Chelsea 0-1 Leicester City na mtupiaji akiwa ni Youri Tielemans ilikuwa ni dakika ya 63 na kuwafanya wasepe na taji hilo mazima.

Usiku wa kuamkia leo, hapohapo Stamford Bridge ubao umesoma Chelsea 2-1 Leicester City ni katika mchezo wa Ligi Kuu England ambao umeongeza nafasi ya Chelsea kumaliza ndani ya nne bora ikiwa itashinda mchezo wake wa mwisho.

Ni Antonio Rudiger alipachika bao la kuongoza dakika ya 47 na la ushindi lilipachikwa na Jorginho dakika ya 66 kwa penalti huku Leicester City wakipata la kufutia machozi dakika ya 76 kupitia kwa Kelechi Iheanacho.

Chelsea ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 67, Leicester City ipo nafasi ya tano na Liverpool ipo nafasi ya nne zote zina pointi 66 hivyo kazi ya kujua nani atamaliza ndani ya nne bora itakamilika baada ya mechi zao za mwisho.


SOMA NA HII  MSIMU WA SOKA LA KIBABE UNAZIDI KUKIMBIZA VILIVYO...SASA NI ZAMU YA LA LIGA...SHIKA 'RIMOTI' YAKO YA DStv KWA NGUVU...