Home Yanga SC SABABU YA MRUNDI WA YANGA KUFELI KUMBE IPO HIVI

SABABU YA MRUNDI WA YANGA KUFELI KUMBE IPO HIVI


NYOTA wa kikosi cha Yanga, raia wa Burundi, Fiston Abdulazack amesema kuwa hapewi nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza jambo ambalo linamfanya ashindwe kuonyesha uwezo alionao kwenye miguu yake katika kucheka na nyavu.

Ingizo hilo jipya kutoka nchini Burundi katika dirisha dogo lilikuwa linapewa nafasi ya kutatua tatizo la ubutu wa safu ya ushambuliaji ila mpaka sasa ameshindwa kuonyesha kile kilichokuwa kinatarajiwa na wengi.

Ni mabao mawili amefunga ndani ya Bongo kwenye mechi za ushindani ambapo alifunga bao moja kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ilikuwa mbele ya Ken Gold ni kwa mkwaju wa penalti.

Bao moja alifunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara zama za Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi mazima.

Nyota huyo amesema:”Unajua nipo Yanga kwa sasa baada ya Kaze kuondoka kumekuwa na mabadiliko kidogo, sipati nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza jambo ambalo linanifanya nishindwe kuonyesha uwezo wangu.

“Ila ikitokea nikapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza basi nina amini kwamba nitafanya vizuri na kila mmoja atajua kwamba ninaweza kufanya kazi vizuri,” amesema.

Chanzo:Spoti Xtra.

SOMA NA HII  NYOTA WAWILI WA YANGA WAREJEA KIKOSINI