Home Azam FC DUBE ANA KAZI YA KUITAFUTA REKODI YA JOHN BOCCO

DUBE ANA KAZI YA KUITAFUTA REKODI YA JOHN BOCCO


NYOTA wa Azam FC Prince Dube ambaye ni namba moja kwa kucheka na nyavu katika Ligi Kuu Bara ameanza kufuata nyayo za watangulizi wake ambao walipita ndani ya kikosi hicho kwa kuwa na mwendelezo mzuri wa kucheka na nyavu.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC kupitia Ukurasa wa Instagram imeeleza kuwa Dube ameweza kufikia rekodi za nyota wengi waliopita katika timu hiyo na ana nafasi ya kufanya vizuri kwa kuwa bado mkononi wana mechi za kucheza ambapo leo Mei 20 watamenyana na Biashata United.

Taarifa hiyo imeeleza namna hii:” Mshambuliaji Prince Dube, anakuwa mchezaji wa kwanza wa Azam FC kufunga mabao 13 kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), baada ya staa wetu wa zamani, Kipre Tchetche


“Tchetche ndiye aliyekuwa mchezaji wa mwisho wa Azam FC kufunga jumla ya mabao 13 kwenye ligi, akifanya hivyo msimu tuliochukua ubingwa wa ligi 2013/2014.

“Dube tuliyemsajili msimu huu, hadi sasa ndiye kinara wa ufungaji mabao kwenye ligi, baada ya kutikisa nyavu za wapinzani mara 13.

“Zikiwa zimesalia mechi tano za ligi ili tuweze kukamilisha msimu huu, Dube anayo nafasi kubwa kuongeza mabao na kuitafuta rekodi ya klabu kwa msimu ambayo ni mabao 19, inayoshikiliwa na John Bocco tangu msimu wa 2011/12.

“Vilevile yupo kwenye nafasi nzuri ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa VPL msimu huu. Azam FC hadi sasa ikicheza msimu wake wa 13 tokea ipande daraja mwaka 2008, imefanikiwa kutoa wafungaji watatu bora, mara 3 mfululizo kwenye ligi.

“2010/11 Mrisho Ngassa, mabao 16, 2011/12 John Bocco, mabao 19 na 2012/13 Kipre Tchetche, mabao 17,” .


SOMA NA HII  AZAM FC WATAJA SABABU YA KUPATA POINTI MOJA MBELE YA NAMUNGO