Home Habari za michezo MAYELE AKUBALI KUMPA FEI TOTO URITHI HUU

MAYELE AKUBALI KUMPA FEI TOTO URITHI HUU

FEISAL SALUM

WAKATI mashabiki na wadau wa soka wakisubiri taarifa ya kuagwa kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele mchezaji huyo amekubali ombi la kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kushangilia kwa kutetema endapo atafunga bao.

Maongezi hayo yamefanyika juzi jioni mastaa hao walitumia zaidi ya saa mbili walipokuwa wanazuingumza kwa njia ya Instagram live.

Ipo hivi; Mayele ameuzwa na Yanga muda wowote anaondoka nchini na kwenda kujaribu maisha mengine nje ya timu hiyo, lakini katika mazungumzo yao na Fei Toto alimuomba kuendeleza staili ya ushangiliaji wake ya kutetema akiwa Chamazi.

“Naomba niendelee kutetema niruhusu kabisa sio nikifunga na kushangilia hivyo unanipigia simu na kuniambia kwanini nafanya hivyo, nipe ruhusa kabisa ili mtetemo uendelee kuwepo;

“Pia nakutakia kila la kheri wewe na familia yako kwenye majukumu yako ya kazi na maisha popote utakapokwenda nitakukumbuka daima,” alisema Fei Toto.

Mayele bila hiyana alimjibu kuwa hakuna shida kufanya hivyo anaamini ataendelea kumuenzi kwa mazuri huku pia akikiri kuwa atakumbuka pasi zake za mwisho ‘asisti’.

“Hapana wewe tetema tu, hamna shida lakini nimefurahi kuzungumza na wewe na nitakumbuka pasi zako pia nakutakia kila la kheri na naamini utakuwa bora zaidi ya vile tulivyokuwa tunacheza pamoja,” alisema Mayele.

SOMA NA HII  MCHAGA WA KILUVYA ALIYESHINDA JACKPOT YA SportPesa.. AKABIDHIWA UBILIONEA WAKE LEO....AFUNGUKA ALICHOFANYA...