Home Simba SC HATMA YA AJIB MIKONONI MWA GOMES

HATMA YA AJIB MIKONONI MWA GOMES


 IMEELEZWA kuwa hatma ya nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu kwa sasa ipo mikononi mwa Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa.

Ajibu ambaye alikuwa bora alipokuwa kikosi cha Yanga, msimu wa 2018/19 alipotoa jumla ya pasi 17 msimu huu kwa sasa amekuwa hana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza ndani ya Simba.

Ilikuwa zama za Patrcik Aussems, ikaja zama za Sven Vandenbroeck na sasa ni zama za Gomes na neno ambalo wamekuwa wakitoa makocha hao ni kama wanaambizana kwa kuwa limekuwa na mlengo mmoja kumtaka mzawa huyo kuongeza juhudi.

Aussems alisema:”Ajibu ni mchezaji mzuri ila anapaswa kuongeza juhudi zaidi ili kuwa bora,” .

Sven alisema:”Ajibu ni mchezaji mzuri ila anatakiwa kuongeza bidii ndani ya uwanja ili awe bora,” .

Gomes amesema kuwa:”Ajibu ni mchezaji mzuri ila ana kazi ya kufanya kuzidi kuwa bora kwa kuongeza bidii na juhudi ili kuwa bora zaidi,”.

Kwa sasa ndani ya Simba Ajibu amekuwa akijenga ushkaji mkubwa na benchi jambo ambalo linafanya maisha yake kutokuwa na uhakika wa kubaki ndani ya Simba.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa mwenye sauti ya mwisho kwa sasa kuhusu Ajibu ni Gomes.

“Ni kocha mwenyewe ataamua kama ataanza na Ajibu ama atahitaji kumpata mbadala wake ambaye atakuwa anamtumia kwani kikosi cha Simba ni lazima kiboreshwe zaidi ili kufikia malengo ambayo yamewekwa,” ilieleza taarifa hiyo.

Gomes kuhusu wachezaji wake hivi karibuni alisema kuwa ambaye atapata namba ni yule ambaye ataonyesha juhudi katika mazoezi.

“Kila mchezaji ana nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza ila lazima afanye juhudi kwa kuwa wachezaji wapo wengi na uwezo wao ni mkubwa,”.

SOMA NA HII  SIMBA KUMTUMIA MISO MISONDO KUWAMALIZA WYDAD KWENYE LIGI YA MABINGWA AFRIKA..