Home Uncategorized AZAM FC YATOSHANA NGUVU NA TRANSIT CAMP

AZAM FC YATOSHANA NGUVU NA TRANSIT CAMP


MCHEZO wa kirafiki uliochezwa leo Uwanja wa Azam Complex kati ya Azam FC ambao walikuwa wenyeji dhidi ya Transit Camp umekamilika kwa timu zote kutoshana nguvu ya bila kufungana.

Mchezo wa leo ni maalumu kwa ajili ya maandalizi ya kurejea uwanjani kwa timu zote ambapo zilikuwa nje ya uwanja tangu Machi 17 baada ya Serikali kuzuia masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuendelea baada ya kueleza kuwa hali ya maambukizi imepungua.

Azam FC Juni 14 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Mbao FC Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wao wa pili, mzunguko wa kwanza Azam FC ilishinda bao 1-0.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA SIMBA, KAHATA ATOA TAMKO