Home Uncategorized NAMUNGO SIO WATU WAZURI WAINYOOSHA NDANDA FC MABAO 2-0

NAMUNGO SIO WATU WAZURI WAINYOOSHA NDANDA FC MABAO 2-0


NAMUNGO FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery leo imewanyoosha kwa mabao 2-0 Ndanda FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Nagwanda Sijaona.

Mchezo huu wa leo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwatazama wachezaji wa timu hizo mbili kuona namna gani wamekuwa fiti baada ya kuanza mazoezi.

Ndanda FC iliyo chini ya Meja, Abdul Mingange inapambana kutafuta nafasi ya kubaki ndani ya ligi huku Namungo ikihaha kutafuta nafasi ndani ya tano bora.

Namungo kwenye msimamo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 28 huku Ndanda FC ikiwa nafasi ya 16  na pointi 31 baada ya kucheza mechi 29.

SOMA NA HII  KITAMBI FULL UBABE GEITA GOLD