Home Uncategorized DAVID MOLINGA ATAJA HATMA YAKE NDANI YA YANGA

DAVID MOLINGA ATAJA HATMA YAKE NDANI YA YANGA


DAVID Molinga, mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga amesema kuwa hana mpango wa kusepa ndani ya klabu hiyo kwa sasa.

Imekuwa ikielezwa kuwa miongoni mwa nyota ambao panga linawahusu msimu ujao ndani ya Yanga ni pamoja na Molinga mwenye mabao nane.

Molinga amesema:”Sitarajii kuondoka kwa sasa ndani ya Yanga labda wakati ujao iwapo mabosi wenyewe wataniambia niondoke ila ninachojua mimi bado ni mchezaji wa Yanga,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kibindoni ina pointi 51 baada ya kucheza mechi 27 za Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  KINDA WA BOUNRERMOUTH ATABIRIWA MAKUBWA MSIMU UJAO NDANI YA LIGI KUU ENGLAND