Home Uncategorized MZUNGU WA AZAM FC ACHEMKA KWA MBONGO HUYU NJE NDANI

MZUNGU WA AZAM FC ACHEMKA KWA MBONGO HUYU NJE NDANI

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union ambaye ni mzawa ndani ya Bongo amemchemsha Kocha bora wa mwezi Januari, Arstica Cioaba raia wa Romania anayeifundisha Azam FC kwa kumpiga nje ndani kwenye Ligi Kuu Bara.
Coastal Union imesepa na jumla ya pointi sita zote mbele ya Azam FC kwa msimu wa 2019/20 kwa kushinda jumla ya mabao matatu huku ikifungwa bao moja pekee na Azam FC ya mzungu Cioaba.
Desemba 26 Uwanja wa Mkwakwani, Coastal Union ilishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ikashinda pia mchezo wa pili wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Februari 15 Uwanja wa Uhuru, Coastal Union ilishinda kwa mabao 2-1. Matokeo hayo yanaifanya Coastal Union kuwa nafasi ya nne ikiwa na pointi 38 huku Azam FC  ikibaki nafasi ya pili na pointi 44 zote zimecheza mechi 22.
Mgunda ameliambia Championi Jumatatu kuwa kikubwa kinachowapa ushindi ni nguvu kubwa ya vijana ambao amekaa nao kwa muda mrefu ndani ya timu.
SOMA NA HII  KAZE: SIMBA BILA CHAMA HAINA MAKALI NDANI YA UWANJA