Home Habari za michezo SIMBA YATANGAZA HALI YA HATARI…IHEFU TUMBO JOTO…ISHU NZIMA IKO HIVI

SIMBA YATANGAZA HALI YA HATARI…IHEFU TUMBO JOTO…ISHU NZIMA IKO HIVI

MASTAA SIMBA WASHIKWA NA NJAA KALI...WAENDELEA KUTEMBEZA KICHAPO

SIMBA imerejea nchini kutoka Morocco ilipoenda kunyukwa mabao 3-1 na Raja Casablanca katika mechi ya mwisho ya Kundi C ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku kocha msaidizi wa timu hiyo, akitamba kwa sasa akili zao zipo kwenye mechi ya ASFC na Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu SC.

Simba itacheza na Ihefu katika mechi ya robo fainali ya ASFC itkayopigwa Ijumaa jijini Dar es Salaam kisha kuifuata timu hiyo nyumbani jijini Mbeya katika pambano la Ligi Kuu Bara na Mgunda alisema pamoja na kupoteza mechi ya CAF wachezaji wameonyesha ukomavu sasa akili yote kwenye mechi mbili dhidi ya Ihefu FC ambao amekiri kuwa ni bora, lakini hawatawaacha salama.

Akizungumza na SOKA LA BONGO, Mgunda alisema wana dakika 180 ngumu dhidi ya Ihefu na mechi zote mbili wanahitaji ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri ikiwamo kutinga nusu fainali ya ASFC na kupunguza pengo la pointi dhidi ya Yanga inayoongoza Ligi Kuu Bara kabla ya kukutana nao.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana Aprili 16 kwenye mechi ya marudiano kwa msimu huu baada ya awali kutoka sare ya 1-1 Oktoba 23 mwaka jana zilipokutana Kwa Mkapa.

Juu ya mechi hizo ikiwamo ya ASFC ikiwa kama wenyeji, Mgunda alisema wanaiheshimu Ihefu kwa vile ni timu ngumu na inayoweza kuwawekea kauzibe kwenye safari yao ya kurejesha ubingwa wa michiano hiyo, lakini anawaamimi vijana wao kutokana na mabadiliko makubwa aliyoona kwa Raja.

“Baada ya kutua wachezaji watakuwa na mapumziko wa siku mbili kuondoa uchovu wa safari baada ya hapo watarudi kambini haraka tayari kwa maandalizi ya mchezo wetu na Ihefu muhimu ni kumheshimu kila tunayekutana naye na kwa hakika zitakuwa dakika 90 za wanaume,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Kitu kikubwa ambacho benchi la ufundi tunafanya hatuwezi kuingia uwanjani na matokeo tunajua kwamba tunaenda kucheza na timu iliyoimarika tofauti na tulipokutana nayo kwenye duru la kwanza la ligi.

“Tumeshazungumza na wachezaji na kukubaliana kwamba hakuna mechi rahisi ya kwenda kuokota tu pointi tatu, ni kweli Ihefu tumewaacha mbali kutokana na uzoefu tulionao lakini haiakisi kiwango chao uwanjani ni timu nzuri tunaifahamu na tutaongia kwa tahadhari nzuri.”

Alisema baada ya mechi ya ASFC watakuwa na siku tatu za kuifuata tena kwenye Uwanja wa Highland Estate, jijini Mbeya na kukutana na dakika nyingine 90 ngumu za Ligi, hivyo watakuwa na wakati mzuri wa kujifua kikamilifu baada ya kurudi kambini kuhakikisha wanakisuka kikosi kimbinu.

β€œTunafahamu ugumu wa kumfunga Ihefu kwenye uwanja wa nyumbani, hatutarudia makosa yaliyofanywa na waliotangulia na tunatambua umuhimu wa pointi tatu mzunguko huu wa lala salama,” alisema Mgunda.

Ihefu iliiduwaza Yanga iliyokuwa imecheza mechi 49 bila kupoteza katika Ligi Kuu kwa kuifunga mabao 2-1 Novemba 29 mwaka jana kabla ya miezi miwili iliyopita ikaibutua Azam FC kwa bao 1-0.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ATANGAZA USHINDI DHIDI YA YANGA....... MVUA YAHUSISHWA