IMEELEZWA kuwa tayari uongozi wa Azam FC umefikia hatua nzuri ya mazungumzo na kocha wa KMC, Etienne Ndayiragije kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho hivyo anahesabiwa masaa tu kutambulishwa.
Ndayiragije ambaye alijiunga na KMC msimu wa mwaka 2018/19 kwa kandarasi ya mwaka mmoja akitokea Mbao imeelezwa amegomea kuongeza mkataba mpya ndani ya KMC.
Akiwa na KMC, ameweza kuonyesha ushindani na kufanya kikosi chake kutisha kwa kuwa ndani ya timu nne bora licha ya ugeni wake ndani ya ligi.
Habari za ndani zimeeleza kuwa mazungumzo ya awali na Azam FC yamekamilika na kilichobaki kwa sasa ni masaa tu ambayo ameambiwa atatambulishwa na uongozi wa Azam FC.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.