Home Habari za michezo WAKATI WENZAKE WAKIWA WANAJIPANGA KUANZA UPYAA..MOSES PHIRI AFUNGUKA SABABU ZA KUWA KWAO...

WAKATI WENZAKE WAKIWA WANAJIPANGA KUANZA UPYAA..MOSES PHIRI AFUNGUKA SABABU ZA KUWA KWAO ZAMBIA…


Mshambuliaji mpya wa Simba, Moses Phiri amesema yupo kwao Zambia kwa mapumziko lakini hajalala kwa vile kila siku amekuwa na awamu moja ya kupiga tizi binafsi ili kujiweka fiti kabla ya kuja kuwasha moto na kikosi hicho cha Msimbazi.

Phiri alisema mara nyingi asipofanya mazoezi na hujipa muda zaidi wa kumpumzika ni rahisi kuongezeka mwili na hilo si upande wake bali wachezaji wote duniani hukutana na tatizo hilo.

Alisema katika awamu hiyo moja ya mazoezi hufanya maeneo mbalimbali, gym, ufukweni mwa bahari na uwanjani akijisimamia mwenyewe ama kuwa na kocha wake binafsi..

“Mazoezi hayo yatanisaidia mara nitakapoungana na timu wakati wa maandalizi ya msimu ujao kwani sitaanza moja kutokana na kupumzika zaidi ya wiki mbili,” alisema Phiri na kuongeza;

“Nikiungana na wenzangu nitakuwa naonyesha kitu nipo tayari kwa ushindani kwani mwili wangu utakuwa umezoea mazoezi tofauti na kuanzia hapo nitaonekana nipo chini. Nafanya hivi na kujiandalia programu yangu maalumu wakati huu kwa siku mara moja ili kuonyesha benchi la ufundi kuna kitu ninacho ili kuaminiwa na kupewa nafasi ya kuipigania timu katika mashindano.

“Wakati nikiendelea na ratiba hiyo napata muda wa kupumzika ili nikiungana na wenzangu niwe na hamu ya kufanya mazoezi pamoja na kucheza mpira nikiamini nitakuwa na mwanzo mzuri.”

Phiri amesajiliwa na Simba kutokea Zanaco ya Zambia, ambaye awali alikuwa wakihusishwa pia na Yanga.

SOMA NA HII  JIWEKE KARIBU NA USHINDI NA JACKPOTS ZA KASINO YA MERIDIANBET....