Home Habari za michezo KUELEKEA KOMBE LA DUNIA…FIFA WAKUBALIANA NA QATAR KUZIFUNGA BAA ZOTE…HAKUNA POMBE KIHOLELA…

KUELEKEA KOMBE LA DUNIA…FIFA WAKUBALIANA NA QATAR KUZIFUNGA BAA ZOTE…HAKUNA POMBE KIHOLELA…


Maboss wa FIFA wamefikia makubaliano na Qatar kuzifunga baa zote kwenye viwanja vya mpira wakati mechi zikiwa zinachezwa.

Taarifa zinasema kuwa mipango bado inakamilishwa lakini majadiliano yaliyofikiwa hadi sasa ni kuwaruhusu mashabiki kununua na kunywa pombe wanapofika uwanjani na wanapotoka.

Aidha kutakuwepo na maeneo mengine kadhaa rasmi ambayo yatatengwa kwa ajili ya kuwapa mashabiki huduma za pombe katika muda maalumu.

Polisi wamejiandaa vilivyo ili kukabiliana na wale wote watakaovunja sheria husika.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA 'AMPIGIA UPATU' MBRAZILI MWENZAKE ASAJILIWE SIMBA...NI YULE GOLIKIPA...