Home Habari za michezo KUELEKEA DABI LEO….GAMONDI ATAJA SILAHA ATAKAYOITUMIA KUIMALIZA SIMBA MAPEMA…

KUELEKEA DABI LEO….GAMONDI ATAJA SILAHA ATAKAYOITUMIA KUIMALIZA SIMBA MAPEMA…

Habari za Simba leo

Kocha wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa falsafa yake anaamini kutumia viungo zaidi kwenye mechi zake kwani ndiyo eneo linaloamua mchezo uchezweje.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza jana na wanahabari kuelekea mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani zao Simba SC, utakaopigwa leo Jumamosi, Aprili 20, 2023 katika Dimba l Mkapa.

“Falsafa yangu inaamini zaidi kwenye kumiliki eneo la Kiungo, ukishika Kiungo umeshika mchezo mzima, unaweza kusema najaza sana watu eneo la Kiungo lakini lazima ujue nawatumiaje Stephen Aziz Ki na Pacome Zouzoua,” amesema Gamondi.

Yanga wana viungo wengi wa kati wakiwemo Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Jonas Mkude, Salum Abubakary Sureboy, Shekhan Ibrahim.

SOMA NA HII  KAMA UTANI KIPA MRUNDI AIBUKIA KAMBINI KWA YANGA