Home Uncategorized SONSO APEWA MAAGIZO

SONSO APEWA MAAGIZO


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, ameamua kumtoa katika nafasi ya ulinzi wa pembeni beki wake, Ally Mtoni ‘Sonso’ kisha kumpa majukumu ya kuwa kiungo mkabaji ambapo atakuwa na kazi ya kuwasaidia mabeki wa kati na viungo.

Kocha huyo amemtoa Sonso ambaye alizoeleka kucheza beki wa kushoto au beki wa kati ambapo alimtumia kama kiungo wa kati kwenye mechi ya ligi kuu waliyocheza dhidi ya Lipuli FC, Jumatano ya wiki iliyopita.

Eymael amemuhamisha namba Sonso baada ya kunogewa kumtumia Jaff ary Mohamed katika upande wa beki wa kushoto pamoja na Adeyum Saleh.

Kocha huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa alimuingiza Sonso katika mechi hiyo na kumtumia kama kiungo wa ukabaji kwa ajili ya kuwasaidia mabeki wa kati na viungo baada ya kuona ana uwezo wa kuhimili kucheza eneo hilo.

“Kwenye ile mechi niliona wapinzani walikuwa wanacheza sana katika eneo la kati ndipo nikamuingiza Sonso kwa sababu ya kuongeza nguvu eneo la ulinzi walipokuwa Makapu (Said) na Moro (Lamine).

“Niliona amefuata kile ambacho nilimuagiza na ukaona kasi ilipungua katika eneo hilo, japokuwa hatukulidhibiti kwa kiwango kikubwa,” alisema Eymael.
SOMA NA HII  SAA 168 ZATENGWA YANGA, HII NDIYO MIKAKATI YAKE CHINI YA MBELGIJI