Home Uncategorized STERLING: UBAGUZI WA RANGI NI UGONJWA UNAOITESA DUNIA

STERLING: UBAGUZI WA RANGI NI UGONJWA UNAOITESA DUNIA


RAHEEM Sterling, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Manchester City amesema kuwa ugonjwa pekee ambao kwa sasa dunia inapambana nao ni ubaguzi wa rangi ambao umekuwa wimbo wa kila taifa.



Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 anayekipiga pia timu ya Taifa ya England, amesema kuwa ataendelea kuzungumza kila wakati ubaya wa ubaguzi wa rangi mpaka pale utakapofika kikomo.

Sterling amesema kuwa watu kwa sasa wapo tayari kwa mabadiliko ndio maana kila eneo wanapambana kuona hali itakuwa salama na wote wakaishi kwa usawa.

Kwa sasa watu wengi wakiongozwa na wale wa Marekani wameonekana wakiandamana kwa amani kupinga kuuawa kwa George Floyd mwenye miaka 46, ambaye inaelezwa kuwa aliuawa na Polisi wa Marekani Mei 25 kwa kile kinachodaiwa ni ubaguzi wa rangi. 


“Najua ni lazima hali kama hiyo itokee,ukweli ni kwamba kwa sasa dunia inapambana na ugonjwa mmoja tu ambao ni ubaguzi na imekuwa ikitokea miaka na miaka. Tunahitaji kutafuta njia ili kusimamisha haya,” amesema.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR : HASIRA ZOTE SASA KWA AZAM FC