Home Uncategorized KAZE: SIMBA BILA CHAMA HAINA MAKALI NDANI YA UWANJA

KAZE: SIMBA BILA CHAMA HAINA MAKALI NDANI YA UWANJA

 




KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa kikosi cha Simba hakina uwezo wa kuwa na makali ndani ya uwanja ikiwa mchezaji wao Clatous Chama hatakuwepo.

Yanga ilishinda kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi mbele ya Simba kwa ushindi wa penalti 4-3 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan Januari 13.

Ndani ya dakika 90 wababe hao walitoshana nguvu bila kufungana na kupelekea kufikia hatua ya matuta ambayo yaliamua nani awe bingwa.

Kwenye kikosi cha Simba hakuwepo Chama ambaye alikuwa amepewa mapumziko na mabosi wake kutokana na kutumia nguvu nyingi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Kaze amesema:”Naona kwamba Simba ni timu nzuri ila inakuwa haina yale makali ambayo yamezoeleka ikiwa hakutakuwa na mchezaji Chama(Clatous).

“Yeye amekuwa akiamua namna ya kucheza na kupeleka mashambulizi, pia ana akili ya kuleta hatari muda wowte hivyo ninaamini kwamba Simba ni timu nzuri ila ikiwa haina Chama inakuwa haina hatari sana ndani ya uwanja,” .

Yanga imetwaa taji lake la pili la Kombe la Mapinduzi na zawadi ya shilingi milioni 15 huku Simba wakiwa ni washindi wa pili na zawadi yao ni shilingi milioni 15.

SOMA NA HII  KINACHOENDELEA BAINA YA YANGA NA FALCAO - VIDEO