Home Habari za michezo MZAMIRU ASHUSHA PRESHA SIMBA SC…

MZAMIRU ASHUSHA PRESHA SIMBA SC…

Habari za Simba sc

KIUNGO wa Simba SC, Mzamiru Yassin amesema bao 1-0 walilolipata dhidi ya Wydad Casablanca limewaaminisha kuwa inawezekana na watafikia lengo lao la kutinga hatua ya nusu fainali CAF wanayoisaka zaidi ya miaka minne.

Simba SC wanatarajia kurudiana na Wydad Casablanca Ijumaa hii wakiwa na mtaji wa ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Mzamiru alisema kitendo cha kumfunga bingwa mtetezi wa ligi ya Mabingwa Afrika ni rekodi kubwa kwao na imewapa nguvu ya kuamini inawezekana.

“Tumeifunga timu kubwa na mimi nikiwa miongoni mwa wachezaji waliocheza dakika zote 90 ni rekodi kubwa kwetu bado tuna dakika nyingine 90 ngumu kuhakikisha tunatinga hatua inayofuata.

“Mengi yanazungumzwa hatuyapi nafasi tunachokiangalia sasa ni namna tutakavyojiandaa kuwakabili kwa dakika nyingine 90 ngumu kwetu tukiwa ugenini lakini tunaamini mwanga upo na tunaweza kufanya kitu kikubwa na cha historia.”

Mzamiru alisema mchezo waliocheza juzi, ulikuwa mgumu na bora kwao matokeo waliyoyapata yamewaongeza nguvu na wameyasahau wanajiandaa kwa dakika 90 za mwisho.

Alitumia nafasi hiyo pia kuwashukuru mashabiki zao kwa kuendelea kuwa pamoja nao huku akiweka wazi kuwa umoja wao waendelee nao wanawapa nguvu ya kupambana zaidi huku akisisitiza kuwa hawajamaliza wanahitaji maombi yao.

“Bado tuna kibarua kigumu ugenini tunajua ni ngumu kuungana nao kwa wingi wao kwenda nao Morocco lakini maombi yao ni muhimu ili twende kukamilisha kazi ambayo tunatamani kuona ikiisha kwa matokeo ya ushindi ili kufikia lengo ambalo tumelishindwa ndani ya misimu minne.” alisema Mzamiru.

SOMA NA HII  CHAMA AZUA GUMZO CCM KIRUMBA .....AFUNGA MJADALA KUHUSU MGOGORO KATI YAKE NA PABLO...