Home Habari za michezo CHAMA AZUA GUMZO CCM KIRUMBA …..AFUNGA MJADALA KUHUSU MGOGORO KATI YAKE NA...

CHAMA AZUA GUMZO CCM KIRUMBA …..AFUNGA MJADALA KUHUSU MGOGORO KATI YAKE NA PABLO…


Presha imetulia, ndivyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki wa Simba kuibua shangwe na kuondoa wasiwasi baada ya kumshuhudia nyota kipenzi wa timu hiyo, Clatous Chama katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Chama hajaonekana kikosini hapo kwa muda mrefu hivyo kuibua wasiwasi kwa mashabiki kutokana na minong’ono kuwa hana maelewano na benchi la ufundi.

Baada ya kutoonekana jana na kikosi hicho katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika uwanja wa CCM Kirumba hatimaye leo Chama ameonekana na kushangiliwa kwa nguvu.

Mzambia huyo aliongozana na wenzake kwa kutumia basi la timu hiyo lililowasili uwanjani hapo saa 8:28 mchana.

Baada ya mastaa wote kushuka kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo huku mashabiki wakijua hayupo hatimaye alishuka na kuwapungia mikono jambo ambalo limeibua shangwe kubwa.

Baada ya kuwasalimia mashabiki Chama alirudi kwenye gari pamoja na Meneja habari wa timu hiyo, Ahmed Ally ambapo  aliendelea kukaa kwenye gari hilo lililopaki uwanjani hapo.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA MIPANGO YAKE KWENYE KIPINDI CHA MAPUMZIKO