Home Habari za michezo FT: GEITA 1-1 SIMBA SC ….MPOLE AZIDI KUTAKATA…KIBU AWAOKOA NA AIBU YA...

FT: GEITA 1-1 SIMBA SC ….MPOLE AZIDI KUTAKATA…KIBU AWAOKOA NA AIBU YA KIPIGO…YANGA SASA BADO NNE TU….


KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta mbele ya Geita Gold Fc mara baada ya kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mcehzo huo ulipigwa kwenye dimba la CCM Kirimba Mwanza.

George Mpole ameendelea kuwa mwiba kwa timu pinzani mara baada ya leo kupachika bao kwenye mchezo huo na kuendelea kufukuziana na Fiston Mayele katika kinyang’anyiro cha mfungaji bora wa ligi.

Simba Sc imeilaisishia Yanga Sc katika mbio za ubingwa ambao mpaka sasa Yanga Sc inahitaji pointi 4 tu itangaze ubingwa kwenye ligi ya NBC.

Bao la Simba limewekwa kimyani na Kibu Dennis nae akiwa ana wakati mzuri katika mechi tano za hivi karibuni.

Kwa matokeo haya, sasa Yanga wanahitaji pointi nne tu kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

SOMA NA HII  KISA AZIZ KI NA DIARRA....GAMONDI ASHUSHA PUMZI YANGA....MPANGO WAKE UKO HIVI...