Home Simba SC GOMES – TUMESHAIMALIZA MECHI DHIDI YA YANGA KITAMBO TU

GOMES – TUMESHAIMALIZA MECHI DHIDI YA YANGA KITAMBO TU


KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema katika mechi tatu za mwisho mara baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu alianza maandalizi ya mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho (ASFC) inayoenda kupigwa Jumapili.

Gomes alisema kwanza alipumzisha wachezaji wake wengi ambao hutumika mara kwa mara katika kikosi cha kwanza na kuwapa programu maalumu ya mazoezi.

Alisema walikuwa wakifanya mazoezi zaidi pamoja na kupumzika ili kuweka miili yao sawa kutokana na kutumika mfululizo na kama ikitokea amepata nafasi ya kucheza fainali na Yanga, awe katika kiwango bora cha kuipigania timu.

“Baadaye nilitoa nafasi kwa wachezaji ambao hawakuwa wakitumika mara kwa mara ili kuonyesha uwezo wao na kwa kiasi kikubwa kila mmoja alifanikiwa kuonyesha hilo kwa kufanya vizuri kutimiza majukumu,” alisema.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao walipewa muda wa kupumzika na kufanya programu maalumu ya mazoezi walikuwa Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Clatous Chama na Luis Miquissone.

Waliopewa nafasi na hakuwa wanatumika mara kwa mara kikosi cha kwanza licha ya Gomes kuwasifia ni David Kameta, Gadiel Michael, Ibrahim Ame, Benno Kakolanya, Said Ndemla, Hassan Dilunga na Meddie Kagere.

Baada ya hapo Gomes alisema kumaliza ligi wakiwa na matokeo mazuri ni wazi hali na morali ya wachezaji itakuwa katika wakati mzuri wa kuhakikisha tunafanya maandalizi ya kutosha ili kushinda fainali.

Gomes alisema licha ya Simba kuonekana kutokuwa na rekodi nzuri dhidi ya Yanga katika kipindi hichi cha karibuni hilo halina shida kwani michezo mingine hakuwepo katika nafasi hiyo.

Alisema anaangalia kwa nafasi yake wameshindwa kupata ushindi katika mechi ya ligi kuna makosa ambayo waliyafanya kwenye sehemu ya maandalizi (mazoezini), pamoja na mechi yenyewe.

“Baada kumaliza mechi ya mwisho na Namungo tulikuwa na mapumziko ya siku moja kisha Jumanne, tulianza mazoezi ya nguvu ili kuwarudisha wachezaji katika hali ya kushindana, mbinu kulingana na upungufu na ubora wa wapinzani wetu walivyo,” alisema Gomes.

SOMA NA HII  BWALYA AZIDI KUNG'AA SIMBA...AKABIDHIWA RASMI MAJUKUMU JOHN BOCCO NDANI YA UWANJA...

“Tunaendelea na mazoezi ya kutosha kuboresha makosa ambayo tuliyafanya katika mechi ya ligi mpaka kufungwa pamoja na masuala mengine ya msingi ambayo si vyema kuweka wazi hapa.

“Nitakaa na wasaidizi wangu tukiwa na runinga pamoja na wachezaji kuangalia namna ambavyo Yanga wanacheza na kuna vitu ambavyo tutavipata hapa ambavyo tutakwenda kuvitumia.

“Tunayafanya yote haya ili kuhakikisha tunashinda mechi hiyo na nina imani itakuwa hivyo ili kutimiza malengo ya timu kutetea ubingwa huo ambao tuliuchukua msimu uliopita.”