Home Habari za michezo WAKATI MASHABIKI YANGA WAKIENDELEA KUMUIMBA….AKILI YA PACOME INAWAZA HILI TU KWA SASA..

WAKATI MASHABIKI YANGA WAKIENDELEA KUMUIMBA….AKILI YA PACOME INAWAZA HILI TU KWA SASA..

FT: YANGA 4-0 CR BELOUZIDAD

Kiungo wa Yanga, Pacome Zouzoua, amesema akilini mwake haiwazi Al Ahly, bali anaifikiria timu watakayokutana nayo kwenye hatua ya robo fainali.

Yanga tayari imeshafuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na pointi nane, lakini bado ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya Al Ahly utakaopigwa jijini Cairo, Jumamosi hii.

Yanga wikiendi iliyopita iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria na kupata nafasi hiyo ambayo ni mara ya kwanza kwao tangu michuano hiyo ianze kutumia mfumo wa sasa mwaka 1998.

Pacome alisema kwa sasa hawana cha kupoteza na maandalizi yake na kikosi kwa ujumla wanaiangalia mechi ya hatua ya robo fainali zaidi.

“Kwangu muunganiko ule umejenga kitu kikubwa sana ambacho hakitasahaulika lakini zaidi kimeongeza morali ya kupambana zaidi na kuhakikisha timu inapata matokeo hata kama nisipofunga mimi.

“Kwa ukweli siwazi sana mechi dhidi ya Ahly imeshakwisha maana tumeshatinga robo fainali, mawazo yangu ni nani tutakutana naye katika robo fainali kwani timu zote ni bora ndio maana zimefika hatua hiyo.

“Naongeza kasi ya kufanya mazoezi magumu ili kuweka mwili sawa huku tukijipanga na mechi hiyo isiyojulikana kwani sitamani kikosi chetu kiishie kwenye hatua hii,” alisema Pacome ambaye mechi dhidi ya CR Belaouzdad ilikuwa maalumu kwake ikiitwa ‘Pacome Day (Kitaalamu Zaidi).

Katika dakika 450 za mechi tano za Ligi ya Mabingwa Afrika alizocheza hatua ya makundi, Pacome amehusika katika mabao matano akifunga matatu na kutoa asisti mbili.

Kiungo huyo katika mechi tano walizocheza za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, amehusika katika mabao matano, huku akifunga mabao matatu kati ya tisa timu hiyo iliyofunga akiwa anashika nafasi ya pili kwa ufungaji wa jumla wa michuano hiyo.

SOMA NA HII  SAIDO ATANGAZA KUFUKUZIA REKODI YANGA